• Breaking News

    Tuesday, February 06, 2018

    Diamond Platnumz, Sikomi Lyrics



    Diamond Platnumz Lyrics


     


    "Sikomi"





    Wanasemaga mapenzi safari


    Unavyopita ndo jinsi unajongea


    Ila niendako ni mbali sijui ka ntafika sababu natembea


    Niliposikiaga habari


    Yakisifika nikakesha nangojea


    Akabariki jalali na nikawika muziki nikauotea


    Ile pruuu mpaka macca


    Nikadandiaga bongo movie


    Kumbe mapenzi hayataki haraka


    Ni kama tango natia tu chumyi


    Mwenzenu nikaoza haswa


    Na kujitia kitandani mjuzi


    Eti nataka fukuza paka


    Badala ya mbwa nikafuga mbuzi, hhhmmm





    Wivu ukanifanya nikagombana na marafiki


    Ugomvi na mamangu akiniambia siambiliki





    Moyo ukanambia nasibu sasa mapenzi basi


    Ila nang'ang'ania najaribu kuipinga nafsi


    Esma ananiambia mdogo wangu mapenzi basi


    Ila nang'ang'ania


    Nikiumizwa na huyu kesho nna mwingine





    Ooh mbona sikomi


    Sikomi


    Sikomi


    Licha ya mateso haya


    Najiuliza (oh sikomi)


    Oh sikomi mbona (sikomi)


    Mbona jamani


    Sikomi


    Licha ya mateso haya, hhhmmm





    Aliyonifanyia wa central


    Haki ya mungu siyawezi sema


    Ila nimejifunza kesho nisiwaamini wacheza sinema


    Moyo walinipatia mateso


    Siwezi kumeza siwezi tema


    Ndio maana sikushanga ile ghafla


    Toka ccm kwenda chadema


    Wanasema kitanda ukitandika sharti ukilalie


    Nikajitia ukamanda yatakwisha


    Wacha nivumilie


    Kila kiza kikitanda


    Ndo visa machozi me nilie


    Penzi yakatia parapanda


    Kuwaita waje washambulie





    Acha na penny we darling


    Nilio muhongaga gari


    Aliponambia ana mimba


    Mwisho wa siku akaichomoa chali


    Mola akanitunuku zari


    Akanzalia dume na mwali


    Niliyvo mjinga nikacheat aibu mpaka


    Kwa vyombo vya habari





    Moyo unanambia nasibu sasa mapenzi basi


    Ila nang'ang'ania najaribu kuipinga nafsi


    Lizer ananiambia simba mapenzi basi


    Ila nang'ang'ania


    Nikiumizwa na huyu kesho nna mwingine





    Ooh mbona sikomi (mbona)


    Sikomi (mbona jamani)


    Sikomi


    Licha ya mateso haya


    Eh nishafumania (oh sikomi)


    Nikafumaniwa mimi (sikomi)


    Nishagombana na watu (sikomi)


    Licha ya mateso haya (mateso haya)







    Lyrics

    Breaking News

    Sports